Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

GOLDEN WOMEN WASHAURIWA KUENDELEA KUWAFIKIA WAHITAJI

15 Jul, 2024
GOLDEN WOMEN WASHAURIWA KUENDELEA KUWAFIKIA WAHITAJI
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, kwa niaba ya Kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha (Golden Women) walipotembelea kituo hicho na kutoa mahitaji mbalimbali, kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake tarehe 14 Julai, 2024.
 
 
Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha, (Golden Women), wameshauriwa kuendeleza utamaduni wa kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu ili kuwasaidia kufikia malengo yao.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi Jenifa Christian Omolo, ametoa ushauri huo  alipotembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD,  kilichopo Kijiji cha Membe, Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
 
Aliongeza kuwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali ni jambo zuri hivyo ni vema utaratibu huo ukaendelea ili kuhakikisha wanawafikia makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji.
 
"Niwapongeze Uongozi wa Golden Women kwa umoja wenu wa kujitoa kwa hali na mali na kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa”alisema Bi. Omolo
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha Bi. Consolatha Maimu, aliahidi kuendelea kuwahamasisha Wanakikundi hao kuwa na utaratibu wa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
 
Naye Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, aliwashukuru  Wanawake wa Kikundi cha Golden Women kwa kufika Kituoni hapo na kupeleka mahitaji .
 
Naye mmoja wa wanufaika wa mahitaji hayo Bi. Florentina Aloyce, aliuomba uongozi wa Kikundi cha Golden Women, kuendelea kuwa mabalozi kwa vikundi vingine ili viweze kufika kituoni hapo ili waweze kupata mahitaji kwa kuwa bado wana mahitaji mengi.
 
Katika kuelekea maadhimisho ya sherehe ya Umoja wa Wanawake, Wizara ya Fedha, imetembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD kwa ajili ya kupeleka mahitaji ikiwemo mahitaji ya shule, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine mbalimbali.
 
MWISHO