Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WAKULIMA NA WAFUGAJI MLANGALI

02 Nov, 2026
ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WAKULIMA NA WAFUGAJI MLANGALI

Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Grace Samwel, akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Mlangali, Wilaya ya Ludewa, kuhusu umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha na vikundi vya kijamii ili kuviwezesha kufanya shughuli za kifedha kwa utaratibu rasmi na kuimarisha usimamizi wa rasilimali zao, wakati wa Programu ya Elimu ya Fedha iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Afya Mlangali Wilaya ya Ludewa.

 

Wakulima na wafugaji wa Kata ya Mlangali, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamepatiwa elimu ya usimamizi wa fedha kwa lengo la kuwawezesha kuongeza tija katika shughuli zao za uzalishaji, kuboresha kipato na kuimarisha ustawi wa kiuchumi.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Afya Mlangali, yametolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) pamoja na Dhamana ya Uwekezaji na Usimamizi Rasilimali Tanzania, (UTT AMIS).

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamejengewa uelewa kuhusu namna bora ya kusimamia mapato, kudhibiti gharama za uzalishaji na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha ili kuhakikisha shughuli zao za kilimo na ufugaji zinakuwa na tija na kuleta manufaa ya kiuchumi.

Aidha, wameelimishwa umuhimu wa kutofautisha fedha za matumizi ya familia na mtaji wa uzalishaji, kupanga matumizi ya fedha kwa ajili ya pembejeo na mahitaji mengine ya uzalishaji, pamoja na kutathmini mapato na matumizi ili kubaini faida inayopatikana.

Vilevile, mafunzo hayo yamewapatia washiriki maarifa ya kuandaa mipango madhubuti ya kifedha kabla ya kuanzisha au kupanua shughuli za kilimo na ufugaji, hatua inayotarajiwa kuwasaidia kutumia rasilimali walizonazo kwa ufanisi zaidi.

Kupitia elimu hiyo, wakulima na wafugaji wanatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia shughuli zao kiuchumi, kuongeza uzalishaji na kipato, pamoja na kujenga msingi imara wa maendeleo endelevu katika sekta za kilimo na ufugaji.

Mwisho