Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA NA WADAU WA MPIRA WA MIGUU WAJADILI MAENDELEO YA SOKA NCHINI

24 May, 2022
DKT. NCHEMBA NA WADAU WA MPIRA WA MIGUU WAJADILI MAENDELEO YA SOKA NCHINI

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na vilabu vya michezo pamoja na taasisi za Serikali zinazosimamia sekta hiyo ili kujadili mipango na mikakati ya kuendeleza sekta ya michezo nchini. 

Wadau hao walimweleza Dkt. Nchemba kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika kuendeleza soka ikiwemo ufinyu wa bajeti katika Vilabu vyao pamoja na kuiomba Serikali iendelee kutoa nafuu zaidi ya kodi kwenye nyasi bandia pamoja na viunganishi vyake.

Dkt. Nchemba amewahakikishia wadau hao kwamba maelekezo ya Mheshimiwa Rais samia Suluhu Hassan aliyowapa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya michezo inakuzwa kwa kuwa ni muhimu na vijana wengi wamejiajiri kupitia sekta hiyo.

Alitoa wito kwa vyama vinavyosimamia michezo nchini kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafanya vizuri ili kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi pamoja na kuhakikisha kuwa miundombinu ya viwanja inajengwa kwenye maeneo ya kimkakati ili kukuza michezo nchini.

Aidha, Dkt. Nchemba amewaangiza wataalum wa Wizara ya Fedha na Mipango wapitie changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wadau pamoja na kuzipitia sharia za kodi ili kuendeleza sekta hiyo wakati huu ambapo bajeti ya Serikali inajadiliwa bungeni.

Akizungumza kwa niaba ya vilabu hivyo vya mpira wa miguu nchini, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Steven Mnguto,  aliishukuru Serikali kwa kuthamini michezo na kuomba changamoto walizoziwasilisha kwake zifanyiwe kazi ili soka la Tanzania liweze kupiga hatua zaidi na kuzipa nafuu klabu ili ziweze kujiendesha.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Fedha ya Mipango