Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AZIOMBA TAASISI ZA DINI KUMUOMBEA RAIS KATIKA KUTIMIZA DIRA YA MAENDELEO

24 Aug, 2022
DKT. NCHEMBA AZIOMBA TAASISI ZA DINI KUMUOMBEA RAIS KATIKA KUTIMIZA DIRA YA MAENDELEO

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba ameziomba taasisi za Dini kuendelea kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuiongoza nchi vizuri na kutimiza dira yake ya uwekezaji katika sekta ya uzalishaji, kutengeneza ajira, kukuza uchumi na kujenga Tanzania yenye umoja.

Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo mkoani Singida aliposhiriki katika jubilei ya miaka 50 ya Jimbo Katoriki Singida.

Alisema Mhe. Rais anadhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo ni vema kumuombea ili yale aliyodhamiria kwa ajili ya nchi yaweze kutimia.

Aidha alisema kuwa taasisi za Dini zinamchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za afya, maji na elimu hususani maeneo ya pembezoni.

Alisema ni vema taasisi hizo zikaendelea kutimiza jukumu hilo ikiwa ni pamoja na kuhubiri amani na umoja miongoni mwa watanzania.

Alisema kuwa kabla dini hazijashamili katika mkoa huo kulikuwa na vitendo vingi vya kihalifu lakini kwa sasa vitendo hivyo vimepungua, hivyo Serikali haiwezi kubeza jitihada za taasisi za Dini katika jambo hilo.

Aidha alitumia jukwaa hilo kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa, jambo litakaloisaidia Serikali kuweka mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji wa wananchi.

Awali Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoriki Jimbo kuu la Dar es salaam, Kardinal Polycarp Pengo, aliwataka viongozi wa kanisa kuwafikiria wengine wenye mahitaji katika kipindi cha miaka 50 ijayo.

Alisema ni kweli Jimbo Katoriki la Singida lilipoanzishwa miaka 50 iliyopita lilikuwa katika hali duni lakini sasa jimbo hilo limekua na kuwa na uwezo wa kuyasaidia majimbo mengine yenye mahitaji pamoja na kushiriki kusaidia jamii

Aidha alisema kuwa mapadri wa mashirika wazawa wa jimbo la Singida wanashiriki kati huduma katika mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi jambo ambalo ni jema kwa kanisa.

Mwisho