Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA ILI KUKUZA AJIRA NA UCHUMI WA NCHI

08 Oct, 2024
DKT. NCHEMBA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA ILI KUKUZA AJIRA NA UCHUMI WA NCHI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiagana na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giussepe Sean Coppola, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo fursa za kuchumi zilizopo katika ushirikiano wa Tanzania na Italia. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali. 
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Italia kutumia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuwekeza mitaji yao katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kukuza uchumi wa pande hizo mbili.
 
Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
 
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeweka vivutio mbalimbali vya uwekezaji na kuialika sekta binafsi ya Italia, kushirikiana na Serikali kwa kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miradi mbalimbali hapa nchini ukiwemo mradi wa Reli ya Kisasa wa SGR.
 
Kwa upande wake, Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, alimwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia vizuri uchumi na maendeleo ya nchi ikiwemo kuunda tume ya kushughulikia changamoto za kikodi nchini.
 
Alisema kuwa anaamini matokeo ya Tume hiyo yataongeza chachu ya kufanyabiashara na uwekezaji hapa nchini hatua itakayochochea ajira, ukuaji wa uchumi na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya nchi.
 
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo kwa kuendeleza mnyororo wa thamani wa zao la kahawa chini.
 
Italia imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali kupitia bajeti kuu ya Serikali, ikiwemo miradi ya maji, afya, mafunzo ya ufundi stadi na huduma katika sekta za utalii na hoteli, uchumi wa buluu na usawa wa kijinsia.
 
Mwisho