Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI WA EAC

25 Jul, 2025
DKT. NCHEMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI WA EAC

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha mashauriano ya ndani kuelekea katika Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika leo tarehe 25 Julai 2025, Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwemo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki), Mhe. Dennis Londo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, utajadili pamoja na mambo mengine, hatua za kikodi zilizo kwenye sheria za fedha za nchi wanachama zenye kuleta athari za kubagua bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi za Jumuiya.

Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa 46 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) na makubaliano ya Mawaziri wa Fedha wakati wa mashauriano ya kibajeti katika mikutano yao iliyofanyika mwezi Mei 2025.