Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AMUAHIDI USHIRIKIANO KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA FEDHA

29 Jan, 2023
DKT. NCHEMBA AMUAHIDI USHIRIKIANO KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA FEDHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amemhakikishia Katibu Mkuu mpya na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El -Maamry Mwamba kwamba Wafanyakazi wa Wizara hiyo watampa ushirikiano wa karibu ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia uchumi wa nchi kwa mafanikio.

Dkt. Nchemba alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha Dkt. Mwamba katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Chamwino, Dodoma.

“Karibu sana!, uko na timu nzuri, nikuhakikishie kuwa watumishi wote wanafanya kazi kitaalamu na hii ni ishara kwamba ni wabobezi katika majukumu wanayofanya” alifafanua Dkt. Nchemba.

Naye Katibu Mkuu mpya wa wizara hiyo na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El -Maamry Mwamba, aliushukuru uongozi wa Wizara na watumishi kwa kumkaribisha.

Aidha, alisema kuwa teknolojia inabadilika kila wakati hivyo aliwashauri watumishi kujenga tabia ya kujiongezea uwezo wa mambo mbalimbali katika kazi zao ili kuongeza ufanisi na kwenda na wakati.

“Sio kwa mantiki ya kusoma shahada ya uzamili au shahada ya uzamivu, ila kuna zile stadi na vitu kwa kuwa dunia inabadilika kila wakati na kwenda na wakati ni vizuri zaidi” alibainisha Dkt. Mwamba.

Kwa upande wao Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo na Bw. Lawrence Mafuru, walisema watampa ushirikiano kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali ili kuhakikisha majukumu muhimu ya wizara yanafanyika kwa ufanisi na weledi.

Nao Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Leonard Mkude na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Athuman Mbutuka walisema kuwa wanaimani na uzoefu na uwezo mkubwa wa kiutendaji aliona nao Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na kwamba ataisaidia nchi kusimamia sera za uchumi ipasavyo.

Dkt. Natu Mwamba, anachukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, ambaye ameteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

 

Mwisho.