Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA MOODY'S

15 Mar, 2023
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA MOODY'S

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia), akisalimiana na Kiongozi wa jopo la wataalam waliowasili nchini kufanya tathimini ya uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Bw. John Walsh, Jijini Dodoma.

 

Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na kuzifanyia tathimini nchi mbalimbali ili kujua uwezo wake wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, Moody’s, imetua nchini kwa ajili ya kufanya tathimini hiyo Tanzania.

Akizungumza wakati akiikaribisha timu ya wataalam kutoka Taasisi hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia Masoko ya fedha ya Kimataifa yatakayoiwezesha nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Amesema kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika licha ya changamoto za Uviko 19 na Vita vya Ukraine na Urusi lakini pia Taifa limepiga hatua kubwa za kiuchumi, kidiplomasia, haki za binadamu na kisiasa.

Dkt. Mchemba alisema kuwa tathimini huru inayofanywa na Taasisi hiyo maarufu Duniani ya Moody’s inaiwezesha Tanzania kuaminiwa na Taasisi za fedha za kimataifa hivyo kuchochea uwekezaji ambao utakuza uchumi wa nchi pamoja na ajira kwa vijana.

Alisema kuwa ujio wa wataalam hao unajibu kiu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeagiza nchi ifanyiwe tathimini ili kubaini uwezo wake wa kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa katika kuharakisha maendeleo ya watu.

 Moody’s inaifanyia tathmini Tanzania kwa njia shirikishi itakayowezesha kutoa taswira halisi ya nchi na hatua ambazo imepiga kiuchumi, kijamii na kisiasa.

 Mwisho