Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA CITIBANK KUJADILI USHIRIKIANO

24 Nov, 2022
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA CITIBANK KUJADILI USHIRIKIANO
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwingulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka CITI Bank Unaosimamia Ukanda wa  Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati , ambapo benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji na kufanya tathimini ya  uwezo wa`nchi kukopesheka (credit rating).
 
Dkt. Nchemba amefanya kikao jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group Bw. David McD. Livingstone amesema Benki yake inajivunia kufanyakazi na Tanzania katika kufikia agenda yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
 
Mhe. Dkt. Nchemba. alielezea kuwa wamejadiliana namna ya kuharakisha ukamilishaji wa suala la tathimini ya uwezo wan chi kukopesheka katika masoko ya kimataifa (credit rating) ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo CITI Group ndio  washauri wakuu wa zoezi hilo. 
 
Alisema kuwa Serikali inaendelea kujadili na kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi mingine ambayo wao wanahusika moja kwa moja kama vile mradi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na miradi mingine ya maendeleo ambayo serikali iliwahusisha katika utafutaji wa fedha ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
 
Dkt. Nchemba alisema kuwa jambo la kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kitaalamu hasa hilo la creding rating pamoja na masuala ya uhamasishaji wa upatikanaji wa rasilimali fedha ambazo Serikali inazipata  kutoka Taasisi mbalimbali za fedha  Benki kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
 
“Tumekubaliana pia katika mazungumzo yetu kwamba wasimamie wito uliotolewa na Mhe. Rais ya kuwaalika wawekezaji kama vile taasisi za kifedha na sekta binafsi kwa kuwa wana mtandao mkubwa katika maeneo tofauti tofauti ili  waje wawekeze na kutumia fursa zilizopo nchini hususan utengenezaji bidhaa ambazo zimepanda bei kama mafuta ya kula, mbolea pamoja na unga wa ngano” alisema Dkt. Nchemba
 
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group Bw. David McD. Livingstone amekukubali kuendelea kushirikiana na serikali kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo na pia kukamilisha zoezi la kutathimini na  kuangalia uwezo wa nchi kuweza kukopa na kulipa madeni na kuhahakikisha kwamba zoezi hilo linakamlika ndani ya muda uliopangwa na kuhamasisha uwekezaji kutoka Sekta Binafsi ili waweze kuchangia maendeleo ya nchi.
 
Mwisho.