Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA AfDB

21 Feb, 2023
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA AfDB

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Bw. Jonathan Nzayikorera, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Bw. Jonathan Nzayikorera.

Dkt. Nchemba amekutana na Mkurugenzi huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, akiwa safarini kuelekea Bujumbura nchini Burundi, kuhudhuria Mkutano wa 43 wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika tarehe 23 Februari, 2023.

Bw. Nzayikorera amewasili nchini leo tarehe 21 Februari, 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine atakagua maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.