Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2024/2025
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

DKT. NCHEMBA AHESABIWA KIJIJINI KWAKE MISIGIRI IRAMBA

24 Aug, 2022
DKT. NCHEMBA AHESABIWA KIJIJINI KWAKE MISIGIRI IRAMBA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka wananchi wote ambao hawajafikiwa na zoezi la sensa kuendelea kutenga muda na pia wakifikiwa watoe ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi

Dkt. Nchemba ameyasema hayo kijijini kwake Misigiri Kiomboi Iramba mkoani Singida baada ya kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi lililoanza rasmi leo tarehe 23 Agosti 2022, nchini kote.

Alisema kuwa ni vema wananchi wote wakatoa taarifa zikiwemo za makundi maalumu wakiwemo walemavu ili taarifa hizo ziweze kumsaidia Mhe. Rais  katika masuala ya kupanga mipango ya maendeleo na utekelezaji wa bajeti.

Dkt. Nchemba amesema kuwa amefurahia zoezi la Sensa kwa kuwa maswali yote aliyoulizwa hayakuwa na utata bali yalikuwa ya maendeleo.

Alisema kuwa karani amekuja kwa wakati na ametumia utaratibu uliozingatia maandalizi ya sensa ya watu na makazi yaliyofanyika.

Mwisho