Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT NATU: TANZANIA NA UNICEF KUENDELEZA USHIRIKIANO

22 Dec, 2025
DKT NATU: TANZANIA NA UNICEF KUENDELEZA USHIRIKIANO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (Kulia), akiwa na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo, walipokutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika hilo hasa katika kutekeleza miradi inayolenga kuinua ustawi wa jamii na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo, ambapo wamejadili kuhusu namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Shirikika hilo hususan maendeleo ya huduma za jamii.

Dkt. Mwamba alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na UNICEF katika kutekeleza miradi inayolenga kuinua ustawi wa jamii na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kwa upande wake, Bi. Patricia Safi Lombo, aliyefika kujitambulisha, Treasury Square jijini Dodoma, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ilizopiga katika kusimamia sekta za kijamii, na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu zaidi katika utekelezaji wa programu za maendeleo zenye tija kwa Watoto.

Mazungumzo hayo yalihitimishwa kwa pande zote mbili kueleza nia ya kuimarisha zaidi uhusiano uliopo, kupitia mipango bunifu inayochochea ustawi wa watoto, vijana na jamii kwa ujumla, sambamba na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

MWISHO