Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NATU MWAMBA ASHIRIKI HAFLA YA WANAWAKE VIONGOZI ILIOANDALIWA NA BENKI YA DUNIA JIJINI WASHINGTON D.C

19 Apr, 2026
DKT. NATU MWAMBA ASHIRIKI HAFLA YA WANAWAKE VIONGOZI ILIOANDALIWA NA BENKI YA DUNIA JIJINI WASHINGTON D.C

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bi. Amina Mohammed (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia masuala ya utawala, Bi. Anna Bjerde (katikati), Waziri wa Fedha wa Lesotho, Dkt. Retselisitsoe Adelaide Matlanyane (wa pili kushoto), na Waziri wa Fedha wa Msumbiji, Bi. Carla Louveira (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kifungua kinywa (women leaders Breakfast) iliyowakutanisha wanawake viongozi kutoka sekta mbalimbali, iliyoandaliwa na Benki ya Dunia, jijini Washington D.C, nchini Marekani kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF inayoendelea jijini humo.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameshiriki katika hafla ya kifungua kinywa iliyowakutanisha wanawake viongozi kutoka sekta mbalimbali, iliyoandaliwa na Benki ya Dunia kupitia Wakurugenzi Watendaji wake, Bi. Anna Bjerde na Bi. Anshula Kant, katika Ofisi za Benki hiyo jijini Washington D.C nchini Marekani, kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF inayoendelea jijini humo.

Tukio hilo limeendelea kukua kila mwaka na kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na maendeleo ya kiuchumi duniani.

Hafla hiyo iliyokutanisha viongozi mbalimbali wakubwa ikiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bi. Amina Mohammed na Waziri Mkuu wa Ukraine, Bi. Yuliia Svyrydenko, ilisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake kiuchumi, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya vijana bilioni 1.2 wanatarajiwa kuingia kwenye soko la ajira katika kipindi cha miaka 10 hadi 15 ijayo.

MWISHO