Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NATU MWAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MIKUTANO YA MWAKA YA BENKI YA DUNIA NA IMF WASHINGTON D.C-MAREKANI

14 Oct, 2025
DKT. NATU MWAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MIKUTANO YA MWAKA YA BENKI YA DUNIA NA IMF WASHINGTON D.C-MAREKANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameongoza ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka (Annual Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), inayofanyika Jijini Washington D.C nchini Marekani, yenye kaulimbiu ya “Foundations for Growth and Jobs”.

Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania nchini humo, Dkt. Mwamba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi na kuahidi kuwa Wizara yake itaendelea kuunga mkono juhudi zake za kusimamia biashara na ukuzaji wa uchumi wa nchi kupitia ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Akiwa Washington D.C, Dkt. Natu Mwamba anatarajiwa kukutana na Viongozi Wakuu wa Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani, akiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga na Makamu wake wa Rais anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Ndiamé Diop, na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Kristalina Georgieva.

Akizungumza katika kikao hicho cha maandalizi ya ushiriki wa ujumbe wa Tanzania katika Mikutano hiyo, Dkt. Mwamba aliwataka wajumbe wote kushiriki mikutano yote kwa weledi na kwa kujitoa kwa hali na mali ili kulinda na kutetea maslahi ya nchi.

Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi kadhaa akiwemo Katibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila.

Wengine ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa, Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fredy Msemwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Frank Nyabundege, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Bw. Deogratius Kwiyukwa, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha,  na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali.