Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWIGULU AKIPONGEZA CHUO CHA MIPANGO KWA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI.

25 Nov, 2023
DKT. MWIGULU AKIPONGEZA CHUO CHA MIPANGO KWA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitunuku shahada wahitimu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini duru ya kwanza Kampasi kuu ya Dodoma katika hafla ya mahafali ya 37 ya chuo hicho, jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekipongeza Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa kuwainua wananchi kiuchumi kupitia Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu cha Chuo hicho (Mipango Enterprenurship and Innovation Centre - MEI), pamoja na miradi inayoendeshwa na wabia wa maendeleo wakiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Fedha katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini duru ya kwanza Kampasi Kuu – Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, amekitaka Chuo hicho kuendelea kutilia mkazo mawazo ya kijasiriamali na ubunifu ya wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha vijana kushiriki kwenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

‘‘Kwa namna ya kipekee ninakupongeza Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Baraza lako la Uongozi  kwa mafanikio ambayo Chuo imeyapata. Mmetoa mchango mkubwa wa kuwainua wananchi kiuchumi kupitia Kituo chenu cha Ujasiriamali na Ubunifu (Mipango Enterprenurship and Innovation Centre - MEI)’’. Alisema Bi. Omolo

Aidha, Bi. Omolo alisema kuwa Serikali imeendelea kuwapunguzia mzigo wazazi wa wanafunzi hasa kwenye suala la kupata elimu hapa nchini kwa kuondoa ada kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita, kuongeza bajeti ya Mikopo ya elimu ya juu kila mwaka.

‘‘Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 731 ikilinganishwa na shilingi bilioni 570 zilizotengwa mwaka wa fedha 2022/23 na Kuanzisha Mikopo ya Elimu ya Stashahada ambapo kwa mwaka wa masomo 2023/24, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 48 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 8,000 wa ngazi ya Stashahada katika fani mbalimbali zikiwemo za Afya na Sayansi Shirikishi’’alisema Bi. Omolo.

Aliongeza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali pia haijawaacha nyuma wahitimu wa ngazi nyingine pamoja na vijana hapa nchini kwani imechukua hatua mbalimbali katika kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujiajiri ikiwemo kuanzisha Programu ya Jenga Kesho iliyo bora (Building Better Tomorrow -BBT), programu ambayo inalenga kuwafungamanisha vijana wasomi na wenzao wengine kwenye kilimo biashara kwa kulima mazao mbalimbali ya kimkakati.

Awali, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya alisema Chuo Kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliandaa Miongozo ya Kufundishia kuhusu miradi inayokopesheka “Bankable Projects” na vyombo maalum vya uendeshaji biashara za taasisi (Special Purpose Vehicle – SPV) kwa Halmashauri zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Halmashauri 13 za Tanzania Bara.

Profesa Mayaya aliongeza kuwa Chuo kilifanya tathmini ya Mkakati wa Kugharamia Utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa kwa kushirikina na Wizara ya Fedha kwa Kukusanya takwimu na uandishi wa ripoti kuhusu tathmini ya Mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu itolewayo na Halmashauri hapa Nchini.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Dkt. Remidius Ruhinduka, alisema Chuo cha Mipango kikiwa ni Chuo pekee hapa nchini chenye jukumu la kuandaa watalaamu wa masuala ya mipango ya maendeleo kitaendelea kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu.

Dkt. Ruhinduka aliongeza kuwa Chuo kitaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali mara kwa mara na kuendelea kutoa wahitimu mahiri na wenye kutumia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) wahitimu 6,362 ambapo wanaume ni 2,783 na wanawake ni 3,579 wametunikiwa Astashahada, Stashahada, Shahada ya kwanza, Stashahada ya uzamili na Shahada ya uzamili.

 

Mwisho