Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2024/2025
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

DKT. MWAMBA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA KITAIFA

15 Mar, 2024
DKT. MWAMBA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA KITAIFA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akizungumza wakati wa kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), kilichowakutanisha Maafisa wa Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali, sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo na Sekretarieti ya TMA, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TBS, TRA, TMX, TIC, TAFA, EPZA, TAHA, Women Chamber of Commerce kilichofanyika jijini Dodoma. 
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, Dkt. Natu El Maamry Mwamba ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) jijini Dodoma ambapo wajumbe walipokea na kujadili hatua iliyofikiwa ya utejkelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Tasisi ya TradeMark Africa (TMA) pamoja na masuala mbalimbali ya kibiashara yenye lengo la kukuza uchumi wa nchi.
 
Kikao hicho kiliwakutanisha Maafisa wa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo na Sekretarieti ya TMA, huku ikijumuisha Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TBS, TRA, TMX, TIC, TAFA, EPZA, TAHA, Women Chamber of Commerce.
 
Aidha Mwenyekiti wa Kikao hicho Dkt. Natu Mwamba alisisitiza taasisi hiyo kuendelea kutekeleza miradi ambayo ina manufaa mapana kwa taifa na inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja
 
MWISHO.