Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA AKUTANA NA BALOZI WA UBELIGIJI NCHINI TANZANIA

21 Jul, 2025
DKT. MWAMBA AKUTANA NA BALOZI WA UBELIGIJI NCHINI TANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo, uliofanyika, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, ambapo wamezungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo. 

Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubeligiji, Bw. Koenraad Goekint na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Ubeligiji, Bi. Fanny Heylen pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Mwisho.