Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA AFRITAC EAST

08 Apr, 2025
DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA AFRITAC EAST

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, baada ya mazungumzo yao kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East, iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linaendesha program ya kuongeza ujuzi katika baadhi ya nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Eritri na Malawi.

Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka.

Mwisho.