Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DENMARK KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

27 Mar, 2025
DENMARK KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, akiagana na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, baada ya kukamilika kwa mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), ukiongozwa na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

Mazungumzo yao yalilenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati. 

Aidha, kupitia Mfuko huo Tanzania inaweza kunufaika na aina mbalimbali za ufadhili unaotolewa na Mfuko huo ikiwemo uwekezaji wa hisa (equity investment), na dhamana (guarantees).

Kikao hicho kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa IFU, anayeshughulikia Sekta ya Umma katika Mikopo Nafuu na Misaada, Bi. Tina Kollerup Hansen, na Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Dhamana, Bw. Theo Ib Larsen.

Kwa upande wa Wizara ya Fedha kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bi. Tiba Kisonga.

MWISHO.