Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

CHEMBA YA WAFANYA BIASHARA SAUDI ARABIA YATAMBUA MCHANGO WA DKT. NCHEMBA KATIKA KUKUZA UWEKEZAJI

18 Dec, 2024
CHEMBA YA WAFANYA BIASHARA SAUDI ARABIA YATAMBUA MCHANGO WA DKT. NCHEMBA KATIKA KUKUZA UWEKEZAJI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lamdeck Nchemba Madelu (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Riyadh, nchini Saudi Arabia, Bw. Ajian Saad Al-jlan, kwa kutambua mchango wake katika kukuza biashara na masuala ya uwekezaji nchini Tanzania, kupitia wadhifa wake wa Waziri wa Fedha. Tukio hilo limefanyika wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Jukwaa lililoandaliwa na Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo, likiwa na lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Saudi Arabia ili kuvutia mitaji na teknolojia vitakavyochochea ukuaji wa uchumi na kukuza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla. 

 

Mawaziri wengine waliotunukiwa zawadi hizo ni Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi Ofisi yar ais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji-Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga.