Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2024/2025
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

CAG KICHERE: BAJETI YA SERIKALI TOLEO LA MWANANCHI LAONGEZA UWAZI

01 Jul, 2024
CAG KICHERE: BAJETI YA SERIKALI TOLEO LA MWANANCHI LAONGEZA UWAZI

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akipewa maelezo kuhusu Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi (Citizen Budget) kutoka kwa Mchumi Mkuu wa Idara ya Usimamaizi wa Bajeti, Bw. Boniface Kilindimo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.

 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa yaliyomo kwenye Bajeti ya Serikali kwa lugha nyepesi (Toleo la Mwananchi) kwa kuwa inamsaidia mwananchi kuielewa bajeti ya nchi.

Bw. Kichere ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa kijitabu hicho ni sehemu ya uwazi na uwajibikaji kwa kuwa mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa mipango ya Serikali katika kutekeleza maendeleo yao.

Aidha, alisema kuwa watoa huduma katika banda hilo wanaonesha umahiri katika kuelezea masuala mbalimbali, jambo ambalo litasaidia kuongeza uelewa kwa umma kuhusu Sera na Majukumu ya Wizara.

Kwa upande wake Mchumi Mkuu wa Idara ya Usimamaizi wa Bajeti, Bw. Boniface Kilindimo, alisema kuwa Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi ni kijitabu kinachotafsiri mipango na bajeti ya Serikali kwa muhtasari na lugha rahisi inayoweza kueleweka kwa mwananchi na wadau mbalimbali.

Alisema kuwa Kijitabu hicho kinasaidia kufahamu mipango na Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka husika na jinsi bajeti inavyoweza kutatua changamoto na kuhamasisha dhana ya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma.

Mwisho.