Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAKUTANA JIJINI BUJUMBURA – BURUNDI

24 Feb, 2023
BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAKUTANA JIJINI BUJUMBURA – BURUNDI

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) wakipitia nyaraka mbalimbali wakayti wa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi– Sekta ya ujenzi, Mhe. Mha. Godfrey Kasekenya (Mb).

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameshiriki katika Mkutano wa 43 wa kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi. Mkutano huo ambao umefanyika baada ya miaka nane (8) toka ulipofanyika kwa mara ya mwisho nchini Burundi umeshirikisha Mawaziri wanaosimamia masuala ya Afrika Mashariki na ushirikiano wa Kikanda pamoja na Mawaziri wenye agenda zinazojadiliwa na Baraza hilo.

Awali kabla ya Mkutano huo kulitanguliwa na vikao vya Wataalamu na Makatibu Wakuu kutoka katika nchi wanachama vilivyofanyika kuanzia tarehe 19 – 22 Februari, 2023 ambao walipitia agenda na mapendekezo mbalimbali ya Jumuiya. Aidha wataalamu hao walipitia taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo ya biashara, forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira, utawala na fedha.

Dkt. Nchemba ameshiriki Mkutano huo pamoja na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambapo watajadili na kupitisha mapendekezo ya agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuitangaza lugha ya Kiswahili kwa kuanzisha vituo vya utamaduni wa lugha hiyo katika Balozi za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa muelekeo wa kuanza kutumika kwa lugha ya Kiswahili na Kifaransa katika uendeshaji wa shughuli rasmi za Jumuiya.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa chini ya Uenyekiti wa Burundi na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchini Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Sudan Kusini umemalizika tarehe 23 Februari, 2023 na maazimio na agenda zilizopitishwa zitawasilishwa katika mkutano wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuridhia utekelezaji wake.  

Mwisho.