Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BALOZI OMAR ATOA POLE KWA MJANE WA MTUMISHI WA WIZARA YA FEDHA.

09 Feb, 2026
BALOZI OMAR ATOA POLE KWA MJANE WA MTUMISHI WA WIZARA YA FEDHA.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza na Bi. Elizabeth Molel, ambaye ni mjane wa marehemu Edwin Emanuel Nalaila, aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ya Fedha, aliyefariki February 5, 2026 jijini Dodoma, alipofika kwa ajili ya kuhani msiba nyumbani kwa marehemu, Makulu Oysterbay, jijini Dodoma.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ametoa pole kwa Bi Elizabeth Molel, ambaye ni mjane wa marehemu Edwin Emanuel Nalaila aliyekuwa mtumishi wa Wizara ya Fedha aliyefariki dunia February 5, 2026 jijini Dodoma.

Mhe. Balozi Omar alitoa salamu hizo za pole alipofika nyumbani kwa marehemu Makulu Oysterbay jijini Dodoma, akiambata na Naibu Waziri wake, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kuungana na waombolezaji wengine akieleza kuwa marehemu alikuwa sehemu ya watumishi wa Wizara waliotoa mchango mkubwa wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara. 

Mhe. Balozi Omar alisema Wizara itaendelea kushirikiana na familia ya marehemu ili kuhakikisha kuwa shughuli za kumpumzisha marehemu zinakamilika kikamilifu.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), alitoa pole kwa familia ya Marehemu Edwin Emanuel Nalaila na kueleza kuwa marehemu alikuwa mchapakazi hodari na kuwa Wizara itaendelea kumkumbuka kwa utumishi wake.

Marehemu Edwin Emanuel Nalaila alikuwa Afisa Tehama Mwandamizi katika Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Huduma za Ndani za TEHAMA, alifariki katika hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma tarehe 5 februari 2026 wakati akupatie a matibabu na anatarajiwa kuzikwa mkoani Arusha.

Mwisho.