Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

AFRIKA KUUNGANA KUCHOCHEA MAENDELEO YA VIWANDA.

24 Jul, 2026
AFRIKA KUUNGANA KUCHOCHEA MAENDELEO YA VIWANDA.

Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akifuatilia mada zilizokuwa zikijadiliwa katika Mkutano wa Pamoja wa 9 wa Kamati Maalum ya Mawaziri (STC) ya Umoja wa Afrika inayosimamia masuala ya Fedha, Uchumi, Mipango na Mtangamano pamoja na Mkutano wa 5 wa Kamati Maalum ya Mawaziri inayosimamia masuala ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, jijini Abidjan, nchini Côte d’Ivoire.

 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pamoja wa 9 wa Kamati Maalum ya Mawaziri (STC) ya Umoja wa Afrika inayoshughulikia Fedha, Uchumi, Mipango na Mtangamano, pamoja na Mkutano wa 5 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara, Utalii, Viwanda na Madini.

Mkutano huo wa kimkakati ulioanza rasmi tarehe 24 Julai 2026 jijini Abidjan, Côte d’Ivoire, unalenga kuweka misingi imara ya ushirikiano wa kiuchumi barani Afrika.

Mkutano huo umejadili kwa kina umuhimu wa nchi za Afrika kuharakisha juhudi za kuendeleza sekta ya viwanda kwa kuongeza thamani ya malighafi za ndani badala ya kusafirishwa zikiwa ghafi, kuimarisha minyororo ya thamani ya kikanda, pamoja na kuweka mazingira bora na wezeshi yatakayovutia uwekezaji wenye tija kiuchumi.

Wajumbe wa mkutano huo walibainisha kuwa, kutokana na Bara la Afrika kuwa na rasilimali nyingi za asili, ardhi kubwa yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, madini ya kimkakati na idadi kubwa ya vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa katika uzalishaji, kuna umuhimu kwa Afrika kuwa kama kitovu cha uzalishaji na biashara duniani.

Aidha, mkutano huo umehimiza umuhimu wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuboresha usimamizi wa rasilimali za asili, na kupambana na ukwepaji kodi ili kukabiliana na pengo kubwa la ufadhili wa maendeleo ya miundombinu ya kisekta.

Mawaziri na wataalamu hao walikubaliana kwa pamoja kuwa maendeleo ya viwanda hayawezi kufikiwa bila uwepo wa mfumo imara wa kifedha utakaowezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu, kupunguza gharama za mikopo, na kuvutia sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.

MWISHO.