Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

ACBF KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU TANZANIA KWA KUAKISI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

16 Apr, 2026
ACBF KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU TANZANIA KWA KUAKISI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida (kushoto), Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Bw. Sosthenes Kewe (kulia), wakimkabidhi kitabu cha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation-ACBF), Bw. Mamadou Biteye, ili kuanza kusaidia mafunzo yatakayotolewa na taasisi hiyo kwa wataalamu wa Tanzania kuakisi Dira hiyo, baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayofanyika, Jijini humo.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ameongoza ujumbe wa wataalamu wa Tanzania katika kikao na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation-ACBF), Bw. Mamadou Biteye, uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayofanyika, Jijini humo, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kuwajengea uwezo wataalamu nchini katika maeneo mbalimbali ya kipaumbele.

Dkt. Mwamba alitoa wito kwa taasisi hiyo kuanza kuwajengea uwezo wataalamu nchini Tanzania ambazo zitaakisi na kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ili kupata ufanisi zaidi na matokeo katika kutekeleza Dira hiyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Bw. Sosthenes Kewe, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga, Meneja wa Uchumi-Jumla kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, Bi. Angela Uforo Shayo, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
 
MWISHO.