Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch (wa tatu kushoto), Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (wa pili kushoto), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule (kushoto), na maafisa wengine waandamizi wa UNICEF, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambacho kilijadili masuala mbalimbali katika kuboresha afya, lishe, elimu na ustawi wa watoto, na utekelezaji wa malengo ya maendeleo yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia), akiagana na Mwakilishi mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Bi. Jana Bricco, aliyefika kujitambulisha tangu ashike nyadhifa hiyo pamoja na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na IMF, ambao umedumu kwa miongo kadhaa tangu miaka ya 1960.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, akizungumza wakati akifungua
kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa tano kulia), Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop (wa nne kushoto), Kaimu Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Firas Raad, na viongozi wengine wa Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa Mkutano wa Kimkakati wa Uwekezaji na Ushirikiano wa Tanzania (Tanzania Strategic Investment and Partnership Forum) uliowakutanisha viongozi wakuu wa taasisi kubwa za kifedha duniani, sekta ya bima na vihatarishi, ulioandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Standard Bank, Jijini London nchini Uingereza.
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa akishiriki mjadala kuhusu nafasi ya sekta ya viwanda inavyoweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi Afrika, mjadala uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa African Caucus wa Mwaka 2026, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia, ambapo amesema kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuchukua hatua madhubiti za kisera na kikodi ili kuiwezesha sekta ya viwanda kuchangia ukuaji wa uchumi, kukuza ajira, kuimarisha uzalishaji na kupanua mauzo ya nje.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb)(katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wanaoshiriki katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea banda la wizara hiyo.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa mijadala ya Mawaziri wa Fedha na Afya wa SADC uliofanyika Harare, Zimbabwe.
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mpya wa Benki ya Afrexim Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Humphrey Nwugo (wa tatu kushoto), na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki ya Afrexim, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), pamoja na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakiongozwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda pamoja na wananchi wakimshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, akizindua rasmi mbio na matembezi ya shukrani kwa walipakodi kuelekea Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora pamoja na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatakayofanyika tarehe 1 Julai 2026, hafla inayolenga kutambua mchango wa walipakodi katika maendeleo ya taifa na kuhamasisha.