KITECHO CHA UKAGUZI WA NDANI (INTERNAL AUDITOR UNIT)

Utangulizi
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni Kitengo ambacho kina jukumu la kutoa  ushauri ili kusaidia Idara zingine ndani ya Wizara ya Fedha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

 


Madhumuni ya Kitengo
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinawajibu wa kufanya kaguzi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na usimamizi wa rasilimali za Wizara na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli unaolenga kuboresha huduma za Wizara ya Fedha ili kufikia Malengo yalivyopangwa.

 


Muundo wa Kitengo
Kitengo kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani akisaidiwa na Wakaguzi wa Ndani watano.

 

Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina majukumu yafuatayo:-

 

  • Kupitia mifumo mbalimbali ya udhibiti (“internal control systems”) na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya uboreshaji wake.
  • Kupanga na kufanya ukaguzi kwa kuzingatia maeneo yenye vihatarishi vitakavyasababisha kutokufikia malengo ya Wizara (High Risk Areas).
  • Kusaidia uongozi wa Wizara kuboresha utendaji ili malengo yaweze kufikiwa kwa kutoa ushauri mbalimbali kama inavyohitajika.
  • Kupitia kanuni, sheria na taratibu mbalimbali zilizowekwa na Wizara/Serikali na kutoa ushauri juu ya utekelezaji wake.
  • Kukagua na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya matumizi, utunzaji na usimamizi wa rasilimali zote za Serikali.
  • Kukagua utendaji/utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kushauri.
  • Kuratibu mafunzo ya kanuni na sheria za fedha manunuzi pamoja na udhibiti wa vihatarishi.
  • Kazi nyingine zinazoelekezwa na Afisa Masuuli.