|
MWELEKEO WA IDARA KATIKA MIAKA 50 IJAYO
Idara inatarajia kufanya mambo yafuatayo katika kuboresha huduma;
-
Mfumo wa malipo wa mishahara ya watumishi wa umma utakuwa umekamilika na umetanuka na kuwawezesha waajiri kuingiza taarifa za watumishi mahali walipo kufikia mwaka 2061. Hivyo udhibiti wa fedha na uwajibikaji utakuwa umeboreshwa kufikia mwaka 2061;
-
Mifumo ya TEKNOHAMA ya Wizara ya Fedha itakuwa imeunganishwa na Mfumo wa Elektroniki wa Serikali “E- Government” kufikia mwaka 2061. Hivyo Ushauri wa wadau utakuwa umehusishwa kikamilifu kufikia mwaka 2061;
-
Shughuli za mitandao ya “Itranet”, “Internet” na kazi nyingine za TEKNOHAMA za Wizara ya Fedha itakuwa imedhibitiwa kufukia mwaka 2061;
-
Utekelezaji wa Mpango mkakati wa TEKNOHAMA “MoF ICT strategy” utakuwa umekamilika kufikia 2061;
-
Huduma za kimuundo na za kiutawala zitakuwa zimetolewa kwa ufanisi kufikia mwaka 2061. Hivyo utendaji kazi wa serikali utakuwa umeboreka kufikia mwaka 2061;
-
Ofisi za Idara zitakuwa zimepewa vifaa vipya vinavyo endana na wakati huo ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Idara kufikia 2061;
-
Mpango wa mafunzo kwa watumishi wa Idara utakuwa umeandaliwa, na kutekelezwa kwa ukamilifu kufikia 2061 ili kuboresha utendaji kazi;
-
Idara itakuwa imepata nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuwaweka wataam wote wa Idara na vitendea kazi kufikia mwaka 2061; na
-
Idara ikizingatia usalama itakuwa imeweka taarifa za malipo ya mishahara kwenye mtandao wa “Internet” ili kuwawezesha wadau kupata taarifa zinazo wahusu mapema kufikia mwaka 2061.
|