Changamoto PDF Print E-mail

Mfumo uliokuwepo kabla ya mwaka 1965, ulikuwa chini ya uongozi wa kigeni (Kiingereza), uliohitaji kuwa na mabadiliko ya uongozi wa kizalendo.

Idara imekabiliwa na changamoto mbalimbali tangu ilipoundwa mwaka 1965, hata hivyo changamoto hizo zilikuwako tangu enzi za Odoleaf unit. Changamoto hizo zimekuwa zikibadilika kadiri muda ulivyokuwa unasonga na nyingine zikipata ufumbuzi wakati mpya zikibuka. Baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa enzi ya Odoleaf Unit ni upungufu wa wataalamu wenye uwezo wa kutumia mashine za odoleaf,upungufu wa wataalamu wazalendo wa kuandika au kufasiri lugha za mashine (programu), ukosefu wa wataalamu wazalendo wenye uwezo wa kitaaluma kusimamia majukumu ya kitengo na hivyo kusababisha serikali kuajiri kwa mkataba wataalamu wa kigeni akiwemo mkuu wa kitengo cha Odoleaf.

Upungufu wa wataalamu wa kompyuta uliendelea kuwepo hadi mwaka 1965 Idara ya kompyuta ilipoundwa, ambapo serikali ililazima au kukodisha wataalamu kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuwapa ujuzi watalamu wazalendo wakati wakifanya kazi pamoja.

Idara haikuwa na kompyuta za kutosha kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya yeke na hivyo Serikali ililazimika kukodi kompyuta kwa baadhi ya nyakati.

Kwa mujibu wa Bwana Patrick Michael Moshi, Kompyuta ya kwanza aina ya 1500 TM iliagizwa kutoka kampuni ya International Computer Tabulator (ICT) ya Uingereza na kufungwa katika Wizara ya Fedha mwaka 1965. Compyuta hii haikuwa na ‘operating system’ na hivyo ilikuwa ikitumia ‘1500 Assembly Language’ hali iliyohitaji wataalamu wengi zaidi na kuchukua muda mrefu kupata zao lililokusudiwa.

Japokuwa kompyuta ya kwanza iliingizwa nchini miaka minne baada ya uhuru, hali ya uuingizaji wa kompyuta nchini haukuwa wa kasi kwa kuwa iligharimu pesa nyingi kuagiza kompyuta na lugha itakayotumiwa na kompyuta ukilinganisha na aina ya kazi itakayofanywa na kompyuta hiyo.

Kutokana na upungufu wa wataalam, ughali wa kuagiza kompyuta pamoja na lugha yake (Machine Language), gharama ya kukodisha kompyuta, gharama ya kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi na ufanisi dhaifu ulipimwa na Serikali katika kutumia kompyuta kwa Idara za serikali nchini, ilidhihirika kuwa matunda yaliyotegemewa hayakuwa yakipatikana. Hali hiyo iliilazimisha serikali kutunga sheria ya kudhibiti uagizaji na uingizaji wa kompyuta mwaka 1974. Kwa Sheria hiyo, haikuruhusiwa kwa mtu au shirika lolote kuagiza na kuingiza nchini kompyuta bila ya kibali cha Waziri wa Fedha. Idara ya kompyuta iliwajibika kumshauri Waziri wa Fedha juu ya maombi yaliyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuingiza kompyuta nchini. Ilikuwa ni lazima serikali iridhishwe kuwa gharama za kuagiza kompyuta zinalingana na aina ya kazi inayotarajiwa kufanywa na kwamba muagizaji ana wataalamu wa kutosha wenye ujuzi wa kutumia kompyuta kwa ajili ya kazi hiyo. Hali hii iliiongezea Idara majukumu na kwa namna moja au nyingine ilizorotesha maendeleo ya kompyuta nchini.

Vitendea kazi vichache visivyolingana na idadi ya wataalamu waliopo Idarani inapelekea Idara kuchelewa kufikia malengo yake.

Kutokuwa na nafasi ya kutosha kuweka vifaa vya ofisi ni changamoto inayopunguza ufanisi wa utendaji kazi wa wataalamu waliopo.

Kuhusiana na usalama wa kuweka kumbukumbu ilikuwa changamoto katika kubuni na kutafuta mbinu mpya ya utunzaji wa kumbukumbu. Kwa mara ya kwanza Idara ilianzisha utunzaji wa data kwenye Magnetic Tapes na disc zilizotunzwa kwenye maktaba maalum.

Majanga asilia kama vile maji ya mvua kuingia ndani ya ofisi na kuharibu vitendea kazi kama kompyuta, nyaraka na kupunguza ufanisi wa kazi

Uaribifu wa binadamu ni kama; wizi au udokozi wa baadhi ya watumishi wasio waaminifu na majaribio ya kutengeneza virusi vinavyoaribu mifumo ya kompyuta.

 
Main page Contacts Search Contacts Search