Mafanikio PDF Print E-mail

Kutokana na ongezeko la watu na mahitaji pamoja na mabadiliko ya Ulimwengu kitekinolojia, kuhusiana na kuandaa taarifa za mishahara na mahesabu mbalimbali. Idara ya kompyuta ilienda sambamba na mabadiliko haya, ambayo tunayachukulia kama mafanikio:

  • Tangu mwaka 1961, muundo wa Idara uliandaliwa na kufanikiwa kuanzisha Idara ya Huduma za Kompyuta mwaka 1965. Idara ilikuwa na sehemu za Computer Operation na Software Development. Idara imefanikiwa katika kuongeza huduma za Kompyuta na Mawasilano na kubadilishwa na kuwa Idara ya Usimamizi na Uratibu wa Mifumo ya TEKNOHAMA. Hii inamaanisha kuwa ni mafanikio makubwa kwa sababu mnamo mwaka 1998, Muundo wa Idara umebadilika kuwa na sehemu (sections) tatu, ambazo ni ‘’Computer Systems Development’’, ‘’Computer Operation na Computer Systems Infrastructure’’ (Miundo Mbinu ya Mifumo).

  • Wakati ule wataalam walikodishwa lakini sasa hivi Idara ina watalamu wazalendo.

  • Huduma za Kompyuta zimeongezeka kutoka kwa watumiaji na waandaaji wa payroll na mifumo mingine pamoja na watumishi wanaotumia kompyuta binafsi. (personal computers) kwenye shughuli mbalimbali. Hivyo tumepunguza gharama za kuwakodi wataalamu kutoka nje ya Wizara.

  • Idara ilianza na technolojia ya mashine code na mpaka sasa tumefikia hatua kutumia ‘’database management systems na compiler software’’, kurahisisha utekelezaji wa kutengeneza mifumo ya Wizara ya Fedha.

  • Kazi ya kutunza kumbukumbu za mishahara, pension, GEPF n.k. kwenye Magnetic tape na disc iliyokuwa ngumu, kwa sasa Idara imefanikiwa kutunza kumbukumbu kwenye Servers, kwa ubora na usalama zaidi.

  • Urahisi wa kazi na taarifa kutoka kwa wakati unaotakiwa kutokana na mabadiliko ya kutoka kwenye mashine zilizofanya kazi kwa kasi ndogo mwanzo na kupata mashine ama kompyuta zinazofanya kazi kwa kasi zaidi.

  • Idara ilianza kazi na watumishi walioajiliwa 30 - 40 na mpaka sasa imefanikikiwa kuwa na watumishi 80.

 
Main page Contacts Search Contacts Search